Serikali yawezesha mapinduzi ya miundombinu mkoani Shinyanga kwa bilioni 221.19

HomeKitaifa

Serikali yawezesha mapinduzi ya miundombinu mkoani Shinyanga kwa bilioni 221.19

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuimarisha juhudi za kuboresha miundombinu ya usafiri kwa kutoa jumla ya Shilingi bilioni 221.19 kwa Mkoa wa Shinyanga.

Fedha hizi zimeelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayojumuisha ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja, makalvati pamoja na usimikaji wa taa za barabarani. Lengo kuu la uwekezaji huu ni kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii, kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji, pamoja na kuongeza fursa za maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo.

Mafanikio yaliyopatikana kutokana na uwekezaji huu ni pamoja na:

  • Kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kutoka kilomita 224 mwaka 2020 hadi kufikia kilomita 281 mwaka 2025
  • Barabara za changarawe zimeongezeka kutoka kilomita 957.11 hadi kilomita 1,411.50
  • Madaraja yaliyopo sasa ni 57, kutoka 45 mwaka 2020
  • Idadi ya makalvati imeongezeka kutoka 2,356 hadi 4,469
  • Taa za barabarani 611 zimesimikwa ili kuongeza usalama kwa watumiaji wa barabara, hasa wakati wa usiku

Utekelezaji wa miradi hii unadhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kujenga uchumi imara kupitia miundombinu bora na jumuishi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Mkoa wa Shinyanga sasa unaendelea kufungua milango ya fursa mpya za maendeleo na uwekezaji kupitia maboresho haya ya kipekee.

error: Content is protected !!