SGR kuanza kutoa mizigo bandarini

HomeKitaifa

SGR kuanza kutoa mizigo bandarini

Serikali imesema kuanzia mwisho wa mwezi huu, itaanza kutumia Treni ya Kisasa (SGR) kusafirisha mizigo moja kwa moja kutoka bandarini, badala ya kutumia bandari ya Pugu kama ilivyokuwa awali.

Hayo yameelezwa baada ta Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kudai kuwa uondoshaji wa mizigo bandarini ni sababu inayofanya ufanisi wa bandari kutoonekana kwa haraka.

Ziara hiyo iliyofanyika wakati TPA ilishuhudia ongezeko la uwezo wa kuhudumia shehena kutoka tani milioni 17 kabla ya maboresho hadi kufikia tani milioni 50.

Akizungumza jana, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alisema Serikali inaendelea kuboresha matumizi ya reli ya kisasa ya SGR na MGR ili kusafirisha mizigo kutoka bandarini kwenda maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani.

Alisema wanajenga kituo cha kutoa mizigo kutoka Bandarini.

“Kuanzia mwisho wa mwezi Machi, MGR itatoa mzigo bandarini, Tazara itasafiri bandarini kuelekea Tunduma na Kapiri Mposhi, Zambi, SGR itaanza kutoka hapa hadi Dodoma,” alisema.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza nguvu treni kwenda Zambia kutoka zaidi ya kilomita 30 kwa saa hadi zaidi ya kilomita 80 na kuongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam dhidi ya bandari nyigine katika ukanda wa Afrika Mashariki.

error: Content is protected !!