Shilingi bilioni 2 za kuwasha majenereta Katavi zaokolewa

HomeKitaifa

Shilingi bilioni 2 za kuwasha majenereta Katavi zaokolewa

Rais Samia Suluhu Hassan ametembela Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme wa Gridi wa Taifa kilichopo Inyonga mkoani Katavi na kisha kuzungumza na wananchi wilaya ya Mlele.

Akizungumza na wananchi hao, Rais Samia amesema ujenzi kituo hicho ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 kwa vitendo kwani iliagiza kufikishwa kwa umeme wa uhakika kwa wananchi.

“Tuliahidi kukamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyote na maeneo ya pembezoni. Ninashukuru kwamba mkuu wa mkoa amesema kazi hii inaendelea vizuri.” amesema Rais Samia.

Kituo cha Kupoza Umeme katika Gridi ya Taifa kilichopo Inyango mkoani Katavi.

Aidha, uwepo wa kituo hicho kunaenda kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 2 zilizokuwa zikitumika kila mwezi kugharamia majenereta yanayowezesha kuwasha umeme mkoani Katavi.

error: Content is protected !!