Mbegu za kiume uhifadhi virusi vya Ebola

HomeKitaifa

Mbegu za kiume uhifadhi virusi vya Ebola

Mwanaume akipata ugonjwa wa Ebola na akafanikiwa kupona, anapaswa kukaa miezi sita bila kujamiiana kwa kuwa virusi vya ugonjwa huo uendelea kuishi kwenye mbegu za kiume kwa kipindi hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Kinga na Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko kutoka Wizara ya Afya, Dk Joseph Hokororo amesema kirusi hicho kinaweza kuishi kwenye maeneo ya maji maji kwa muda wa miezi sita, na eneo kavu kinaweza kuishi kwa saa kadhaa.

Amesema mbali na kwenye mbegu za kiume pia kirusi hicho kinauwezo wa kukaa kwenye Kondo la Nyuma la Mama (Placenta).

Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa.

Akizungumza anasema “Ugonjwa wa Ebola uua kwa asilimia 40, hii maana yake ni kuwa kati ya watu 100 waliogua Watu 40 mpaka 90 wanapoteza maisha.”Amesema na kuongeza

“Iwapo mwanaume akabahatika kupona basi anapaswa kukaa miezi sita bila kukutana na mwanamke kwa kuwa licha ya kupona kirusi hicho kitaendelea kuishi kwenye mbegu zake za kiume kwa miezi sita hivyo akikutana kimwili na mwanamke atamuambukiza Ebola.”Amesema Hokororo

error: Content is protected !!