Uhalali wa matumizi ya bangi nchini

HomeKitaifa

Uhalali wa matumizi ya bangi nchini

Mamlaka ya kudbihiti na Kupamabana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema haiwezi na haina mamlaka ya kuruhusu matumizi ya bangi nchini kwa kuwa jambo hilo ni mtambuka ambalo linatakiwa kushirikisha wadau wengi kufukia uamuzi.

Aidha, mamlaka hiyo imeonya watu kutotumia kigezo cha kwamba Rais Samia Suluhu amefungua nchi kwa kuanza kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya, alisema hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na luninga ya ITV.

“Suala la kuruhusu bangi ni jambo ambalo ni mtambuka linatakiwa kuhusisha wadau wengi. Sisi kama mamlaka tunaweza kuwa wadau wa mwisho kabisa sababu sisi kazi yetu ni kudhibiti na siku zote huwezi kuruhusu matumizi ya bangi kabla hujafanya utafiti,” alisema.

Kuhusu watu kudai Rais amefungua nchi kwa hiyo wanaweza kufanya lolte, alisema Rais amefungua nchi ina maana ni katika mambo yanayoruhusiwa na kukubalika kisheria.

“Suala la bangi haliwezi kuwa sehemu ya kufungua nchi, haramu itaendelea kuwa haramu mpaka pale ambapo kutakapohalalishwa na mamlaka zinazohusika,” alisema.

error: Content is protected !!