Somalia yashinda mgogoro wa mpaka na Kenya

HomeKimataifa

Somalia yashinda mgogoro wa mpaka na Kenya

Mahakama ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa (ICJ) imetoa hukumu juu ya mgogoro wa bahari kati ya Somalia na Kenya, eneo ambalo linasemekana kuwa na utajiri mkubwa na rasilimali za mafuta ya gesi.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo kwa kuipa haki Somalia juu ya eneo kubwa lenye utajiri katika Bahari ya Hindi. Mahakama hiyo kwenye hukumu yake imesema kuwa awali hakukuwa na mpaka unaotambulika kwenye eneo hilo, hivyo mahakama imeamua kuchora mpaka mpya ambao umechora karibu zaidi na eneo ambalo Somalia ilikuwa ikidai ni lakwake.

Uamuzi huo ni halali kabisa, ingawa changamoto kubwa ya mahakama hiyo, haina nguvu ya kushinikiza utekelezaji wa hukumu hiyo.

Mahakama imekana madai ya mpaka ambao Kenya imekuwa ikiudai, na pia Mahakama imetupilia mbali madai ya Somalia ya kutaka kulipwa fidia na Kenya, wakishutumu kuwa baadhi ya shughuli za Kenya ndani ya mipaka ya Somalia imeingia uhuru wa Taifa hilo.

Kenya imekana vikali hukumu hiyo na kusema kuwa imetolewa kwa upendeleo kwa Somalia.

Somalia ilifungua kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya (ICJ) mwaka 2014 ambapo kesi hiyo iliibua mgogoro wa kisiasa kati ya mataifa hayo mawili.

error: Content is protected !!