Star wa Series ya “Empire”, Taraji sasa kuhamia kwenye muziki

HomeBurudani

Star wa Series ya “Empire”, Taraji sasa kuhamia kwenye muziki

Mwigizaji nyota toka nchini Marekani, Taraji Henson, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni kupitia ‘Series’ ya Power, ametangaza rasmi kuanza kufanya muziki huku akisema kwamba ataanza kwa kuachia EP yake aliyoipa jina la “FEEL GOOD MUSIC” iliyo mbioni kumalizika.

Taraji amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Good Morning America’ kwamba ameamua kuanza kufanya muziki sababu ni kitu anachokipenda tangu zamani hivyo ameona ni wakati sahihi kufanya muziki

Nyota huyo amejipatia umaarufu kwenye filamu na thamthilia mbalimbali kama Empire, Person of Interest, ‘What men want’, ‘The Karate Kid’, Coffee and Karem, Proud Mary na nyingine nyingi. #clickhabari #burudani

error: Content is protected !!