Steve : Natoa masaa 48

HomeBurudani

Steve : Natoa masaa 48

Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), Steve Nyerere ametoa masaa 48 kwa Mbunge wa Muheza, Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA na wasanii wote waliokaa kwenye kikao jana ili kujadili uteuzi wake wa cheo hicho.

“Kama msemaji wa industry (kiwanda) ya wanamuziki Tanzania nampa masaa 48 tena hili nipo serious nalo, nikirudi hapa patachimbika . Nampa masaa 48 awaombe radhi wale wote aliowafedhehesha Watanzania,” alisema Steve.

Akizungumza na waandishi wa habari, Steve Nyerere alisema kati ya watu waliotenda makosa ni Mwana FA akidai kuwa yeye kama kiongozi mwenye nguvu serikalini alikuwa na uwezo wakuwaunganisha wasanii hao katika kufikia muafaka mzuri na sio kujigawa.

“Mimi nilidhani kabisa kwa akili zangu niliamini kabisa kikao kile kama kimeongozana na mtu mwenye power (nguvu) serikalini basi alitakiwa awe daraja kwetu la kutuunganisha, nichukue nafasi hii kumuombea radhi kokote kuliko huko alipo,” Steve Nyerere.

Aidha, Steve alisema yeye hawezi kujihudhuru mpaka viongozi wa shirikisho hilo watamfata kwa barua kama ambavyo walimfata mara ya kwanza kumuomba awe msemjai wao.

“Nitajihudhuru kama mwenyekiti, makamu mwenyekiti, bodi ya shirikisho watakaa kama walivyoni-approach kuniletea barua tukakaa vikao, nitatoka hadharani kusema hili ndugu zangu naachia ngazi,” alisema Steve Nyerere. 

error: Content is protected !!