Kaburi la vijana wengi

HomeElimu

Kaburi la vijana wengi

Vijana wengi wamekuwa wakishindwa kutoka kwenye kaburi la kupata mafanikio na kusonga mbele katika maisha na hii ni kutokana na kuwa ndani ya kifungo hicho kwa muda mrefu bila kujua.

Kama umemuona mtu kasoma mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri siyo kwamba amekuzidi. Ni namna tu alivyoweza kuyashinda baadhi ya mambo wakati anaanza kutimiza ndoto zake. Fanya haya kutimiza ndoto zako:

Ishinde hofu ndani yako

Ile sauti inayokuambia huwezi kuwa rubani, huwezi mfanyabiashara mkubwa ndiyo ya kuikataa. 

Sauti hiyo inaweza kukufikirisha na kukuibulia changamoto nyingi ambazo zinakuzunguka , siyo rahisi kwa wewe kutoboa. Kataa sauti hiyo na usikubali changamoto zikukwamishe. 

Chukua hatua

Baada ya kuishinda hofu hiyo ndani yako, chukua hatua maana yake anza kufanya vitendo ili uweze kufikia ndoto zako.

Anza pale ulipo, usiangalie kazi iliyopo mbele yako ambayo unadhani itakufanya utumie rasilimali nyingi kukamilisha ndoto yako. Kama ni biashara, anza na hata ya mtaji mdogo kabisa lakini lenga kufika mbali. 

Usikate tamaa

Usiwasikilize wanaokurudisha nyuma bali shikamana na watu ambao wanakutia moyo kufika mbali kimaisha.

Wakati unatimiza ndoto yako, utakutana na watu au mambo ambayo yatakuvunja moyo na kukukatisha tamaa ili usifike kule unakotaka kwenda. Katika mazingira yoyote yale usikubali kurudi nyuma na kuacha ulichoanzisha. Kila jema lina ugumu wake kulipata.

Usipoteze muda

Ndoto za watu wengi zimekufa au zimechelewa kutekelezeka kwa sababu walipoteza muda wakati wanaanza au hawakutumia muda vizuri kwa kila hatua waliyopiga.

Weka malengo ya kutimiza ndoto zako yanayoendana na muda yaani fanya kila jambo kwa muda fulani ili kusogea mbele. Pia jiwekee muda maalum wa kufikia ndoto zako hata kama unahisi huwezi kutimiza kwa wakati huo. Hii itakuongezea kasi na bidii kufika kwa uharaka kule unakokwenda.

error: Content is protected !!