Mtoto alawiti wenzake 19

HomeKitaifa

Mtoto alawiti wenzake 19

Mtoto mwenye umri wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) mkazi wa Manispaa ya Iringa, anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuwalawiti watoto wenzake 19 kwa nyakati tofauti akitumia pipi, juisi na biskuti kuwalaghai.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo na kusema mtoto huyo aliwafanyia wenzake watatu na baada ya uchunguzi iligundulika walikuwa watoto 19.

“Baada ya kuwapata watoto hao watatu pamoja na mtuhumiwa walizalisha taarifa ambayo ilibaini kwamba jumla ya watoto waliokuwa wamelawitiwa na mtuhumiwa ni 19,”alisema Kamanda Bukumbi.

Baada ya kuhojiwa mtoto huyo alisema alianza kufanya vitendo hivyo tangu mwaka 2019 na kutaja sehemu ya jirani na nyumba yao ndipo alikokuwa akiwalawiti wenzake.

Akieleza namna alivyowarubuni watoto hao ni kwamba walikuwa wanakwenda kuangalia televisheni na alikuwa na uwezo wa kupata fedha kutoka kwa bibi yake aliyekuwa akiishi naye.

 

error: Content is protected !!