Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limetoa ufafanuzi wa picha mjongeao (video clip) iliyoonekana kusambaa kwenye mitandano ya kijamii ya Aprili 20, 2025 ikimuonyesha mwanamke mmoja aitwaye Slvia Vlaskamp mkazi wa Moshi mmiliki mwenza wa Kampuni ya VASSO AGRO VENTURES akilalamika kunyanyaswa kikatili na Askari wa Kampuni Binafsi pamoja na kufungiwa ndani ya nyumba yake na kuibiwa vitu vyake.
Kupitia taarifa yake kwa Umma, Jeshi la Polisi limeeleza kwa kina tukio hilo na kufafanua kilichotokea.
UFAFANUZI KUFUATIA PICHA MJONGEO INAYOMWONESHA MWEKEZAJI AKIDAI KUNYANYASWA NA MLINZI WA KAMPUNI BINAFSI MKOANI KILIMANJARO pic.twitter.com/QmFC4LBQYX
— Police Force TZ (@tanpol) April 21, 2025