Taarifa ya ACT Wazalendo kuhusu kauli ya Bernard Membe

HomeKitaifa

Taarifa ya ACT Wazalendo kuhusu kauli ya Bernard Membe

Siku chache baada ya aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania mwaka 2020 kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe kusema kuwa anaunga mkono utendaji utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba yuko njiani kurudi (hakuweka wazi kurudi wapi), chama hicho kimesema suala zima linalomhusu mwanasiasa huyo lina mafunzo mengi.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Addo Shaibu amesema kwamba Membe alipojiunga na chama hicho walimpa nafasi ya kugombea kwa sababu waliamini alikuwa mpinzani dhidi ya iliyokuwa serikali ya Hayati Dkt. John Magufuli.

“Tulikuwa tunamuona kana kwamba ni mpinzani ndani ya CCM [Chama cha Mapinduzi], kwa hiyo tukampa nafasi lakini baadaye yaliyotokea yametokea na kuja jambo tumejifunza,” amesema Shaibu.

> Membe amuomba kazi Rais Samia

Amesema kwamba moja ya mambo ambayo ni muhimu wanasiasa kujifunza ni msingi wa kuheshimiana katika kipindi cha Migogoro. Amesema tangu walipopishana na Membe kwenye mambo kadhaa na baadaye mwanasiasa huyo kujivua uanachama, hakujatolewa taarifa rasmi ya chama kumkosea heshima au kumtukana, na wala Membe hajafanya lolote kukivunjia heshima chama hicho.

“Ndio maana mara nyingi mkituuliza masuala ya Membe tunamtakia tu kila la heri,” ameongeza.

Membe alijiunga rasmi na ACT Wazalendo Julai 2020 na baada ya kufukuzwa uanachama CCM, lakini baadaye alijivua uanachama wa ACT Wazalendo Januari 1 mwaka huu.

error: Content is protected !!