Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 12 (Lacazette mbioni kuachana na Arsenal, huku safari ya Hazard kurudi Chelsea imepamba moto)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 12 (Lacazette mbioni kuachana na Arsenal, huku safari ya Hazard kurudi Chelsea imepamba moto)

Klabu ya Liverpool inamfuatilia kwa karibu winga wa Barcelona Ousmane Dembele, 24. Mkataba wa mchezaji huyo wa unamalizika mwisho wa msimu huu (Mundo Deportivo – Spanish).

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette (30) hana mpango wa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo pale mkataba wake wa sasa utakapokwisha mwisho wa msimu huu (Football London).

Lucien Favre 63, aliyekuwa kocha wa Borussia Dortmund  na Frank Lampard 43,  wanatajwa sana na wamiliki wapya wa Newcastle United ambapo wanapendelea mmoja wao achukue nafasi ya kocha Steve Bruce (Telegraph).

Aaron Ramsey 30, bado anaamini anaweza kufanikiwa Juventus akiwa amesalia na msimu mmoja na nusu katika mkataba wake wa sasa (Times).

   > Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 11 (Morata kuchukua nafasi ya Kane Tottenham, Adama Traore akinyatiwa na Liverpool)

Kiungo wa kati wa PSG Georginio Wijnaldum (30) anasema “hajafurahia vilivyo” maisha yake katika klabu hiyo. Ikiwa miezi minne imepita sasa tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka Liverpool (Independent).

Klabu ya Juventus imeanza mazungumzo na wakala wa Donny van de Beek 24, wa Manchester United, lengo lao ni kumsaji mchezaji huyo (La Stampa via Football Italia).

Juventus pia wanajiandaa kumsajili kwa mkopo nyota wa Manchester City Bernardo Silva 27, mwezi Januari dirisha dogo la usajili litakapofungliwa (Calciomercato – Italian).

Manchester United huenda wakamuuza kiungo wa kati mshambuliaji Jesse Lingard, 28, kwa kima cha pauni milioni 15 mwezi Januari ikiwa hatasaini mkataba mpya Old Trafford, mkataba wake wa sasa unaisha msimu ujao (Sun).

Klabu ya Chelsea imefanya mazungumzo rasmi na Real Madrid juu ya kumsajili tena Eden Hazard (34), lakini klabu hiyo ya Uhispania inamtaka Reece James 21, kuwa sehemu ya usajili huo (El Nacional).

 

 

error: Content is protected !!