Tanzania haidaiwi zaidi ya sh. trilioni 10 na EIB

HomeKitaifa

Tanzania haidaiwi zaidi ya sh. trilioni 10 na EIB

Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania imewataka wananchi kupuuzia taarifa zinazoonekana kupitia mitandao ya kijamii kuwa Serikali inadaiwa Dola za Marekani bilioni 4.1 za Marekani (zaidi ya Sh9.594 trilioni) na Benki ya Umoja wa Ulaya (EIB).

​Kupitia ukurasa wa Twitter unaotambulika kama Tanzania Abroad Tv, Machi 5 mwaka huu ulichapisha taarifa hiyo ikiwa imeambatana na barua kutoka EIB inayoonesha madai hayo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja katika taarifa yake aliyoitoa Machi 6 mwaka huu amesema mara kwa mara ukurasa huo umekuwa ukitoa taarifa za uzushi, upotoshaji na uzandiki kuhusiana na wizara hiyo na Serikali kwa ujumla.

“Tunawaomba Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa mpuuze taarifa hizo, ambazo hazina ukweli wowote na kwa vyovyote zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki zisizo na msingi, “ inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa pamoja na kuwa EIB ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na ina mahusiano mazuri na Serikali haina mkopo wa kiasi kilichotajwa ma mtandao huo.

Mwaipaja amewakumbusha na kuwaonya wamiliki na watoaji wa habari kupitia mitandao ya kijamii kuepuka kuchapisha habari za uzushi, na potofu kwani ni kinyume na Sheria ya Vyombo ya Habari ya mwaka 2016.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Wizara ya Fedha Na Mipango (@urtmof)

error: Content is protected !!