Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imefanya uchunguzi wa taarifa ya kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2023, Abdalah Shaibu ambaye aliikataa miradi 20.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Hamduni amesema hayo leo Machi 28 IKulu Chamwino akiwasilisha ripoti ya taasisi yake, ambapo Rais Samia anapokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2022/2023 pamoja na ripoti ya Takukuru.
Hamduni amesema katika majalada 20 ambayo yalichunguzwa, majalada 12 uchunguzi wake ulikamilika, jalada moja mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na ameshahukumiwa baada ya kupatikana na hatia, jalada linguine moja limehamishiwa Polisi, majalada nane uchunguzi unaendelea na mengine yapo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Amesema Takukuru ilifungua kesi mpya 600 mahakamani kati ya hizo kesi 594 zilifunguliwa katika mahakama ya chini na kesi sita zilifunguliwa Mahakama Kuu.