Rais Samia asamehe faini za bili za maji

HomeKitaifa

Rais Samia asamehe faini za bili za maji

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassani ameelekeza Wizara ya Maji kupitia Mamlaka za Maji kutoa hamasa kwa Wateja wake kwa kusamehe madeni yao na kuondoa faini kwa kipindi cha mwezi mmoja na kwamba Mteja atatakiwa kuwajibika kwa kulipia sehemu ya deni lake halisi tu kidogokidogo na pia arejeshewe maji huku akiendelea kufurahia huduma ya upatikanaji wa majisafi na salama.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema hilo leo March 26,2024 Jijini Dodoma akiwa kwenye kikao kazi na Viongozi wa Watendaji wa Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na Menejimenti ya Wizarq Maji, Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka zote za maji pamoja na Mameneja wa Mikoa Maji Vijijini RUWASA kwa lengo la kuendelea kukumbushana na kuelezana kwa msisitizo wajibu wa Sekta katika kufanikisha utendaji kazi, utoaji huduma na utekelezaji wa miradi ya maji inayoendelea hapa Nchini..

“Tunatoa mwezi mmoja Mwananchi ambaye umekatiwa maji kwasababu ya faini umechelewa kulipa na umekatiwa maji, faini tunasamehe kwa mwezi mmoja kupitia maelekezo ya Mh. Rais, sasa chelewachelewa utamkuta Mwana sio wako, hata kama una kideni kikubwa niwaombe Watendaji wekeni utaratibu ili Mtu awe anapunguza kidogokidogo huku anapata huduma”

Aweso amewataka pia Watendaji wote wa Mamlaka za Maji na Bodi zake kuwa kipimo cha ufanisi katika kazi kitakua katika maeneo ya kudhibiti upotevu wa maji pamoja na kutochelewesha maunganisho mapya kwa mteja mwenye kutaka huduma ya Maji.

SOURCE: MillardAyo

error: Content is protected !!