Tamko la Pamoja Laweka Msingi wa Ushirikiano Mpya wa Kilimo kati ya Tanzania na Malawi

HomeKitaifa

Tamko la Pamoja Laweka Msingi wa Ushirikiano Mpya wa Kilimo kati ya Tanzania na Malawi

Tanzania na Malawi zimefikia makubaliano muhimu ya kurejesha na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baada ya kikao cha kihistoria cha mawaziri kutoka sekta za Mambo ya Nje, Kilimo, Viwanda na Biashara kilichofanyika jijini Dodoma.

Makubaliano hayo yametiwa saini kupitia Tamko la Pamoja lililowekwa na mawaziri kutoka pande zote mbili. Waziri wa Kilimo wa Malawi, Mhe. Sam Kawalenga, alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kwenye majadiliano hayo yaliyolenga kufungua fursa mpya za kibiashara na kuimarisha mahusiano ya muda mrefu baina ya mataifa haya jirani.

Makubaliano hayo yanalenga kukuza biashara katika sekta ya kilimo, kuboresha maisha ya wakulima na kuzingatia mikataba ya kikanda na kimataifa. Hatua hii ni ushahidi wa maendeleo ya diplomasia ya kiuchumi inayojikita kwenye mafanikio ya wakulima na maendeleo endelevu ya kiuchumi.

error: Content is protected !!