TANESCO Pwani yavuka lengo

HomeKitaifa

TANESCO Pwani yavuka lengo

Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Pwani limeunganishwa wateja 43,000 na kuvuka lengo la kuunganishia wateja 20,000 kipindi cha mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Pwani, Mahawa Mkaka alisema wateja hao ni wa wilaya zote za mkoa huo.

Mkaka alisema kwa mwaka wa fedha wa 2023, wamejipanga kuunganisha wateja 30,000 ifikapo Juni 30 na hadi sasa wameunganisha wateja 12,000.

“Kwa sasa tuko vizuri kwani vifaa vyote vipo kuanzia mita, transfoma, nguzo na nyaya hivyo hakuna mteja kuchelewesha hivyo wateja waje kwa wingi watapata huduma kwa wakati,” alisema.

Mkaka alisema kwa sasa mteja anaunganishwa kwa muda wa siku nne au wiki moja kwani vifaa vipo vya kutosha.

error: Content is protected !!