Tanzania imekuwa nchi bora yenye uhuru wa vyombo vya habari katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan yaliyoleta mageuzi makubwa.
Ripoti ya Reporters Without Boarders (RWB) inaonyesha kwamba Tanzania imepanda viwango kutoka nafasi ya 143 hadi nafasi ya 97 mwaka 2024.
Kupanda kwa viwango kunatokana na hatua zilizochukuliwa na Rais Samia za kubadilisha mwelekeo wa nchi ndani ya miaka yake mitatu ya uongozi na kuondoa vizuizi vya uhuru wa habari vilivyokuwepo.
Baadhi ya mabadiliko yaliyofanyika ni pamoja na kufungulia na kuviachia huru vyombo vya habari vilivyofungwa, mabadiliko ya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari 2016 na Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta (EPOCA) 2010.
Uhuru wa Vyombo vya Habari ya Dunia ya Mwaka 2024:
Tanzania – 97
Kenya – 102
Burundi – 108
DR Congo – 123
Uganda – 128
Sudan Kusini – 136
Rwanda – 144
Somalia – 145