Kwa mujibu wa taarifa ya Transparenncy International kwa kutumia kiashiria cha The Corruption Perceptions Index (CPI), Tanzania imekuwa nchi ya pili kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi cha vitendo vya rushwa kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mhe. Crispin Chalamila, wakati akiwasilisha taarifa ya mwaka ya utendaji TAKUKURU mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Crispin Chalamila.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo inathibitisha kuwa juhudi za serikali kuimarisha mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika kufanikisha malipo na utoaji wa baadhi ya huduma, zimeleta mafanikio katika mapambano dhidi ya rushwa.