Tanzania imenufaika na Michuano za Kombe la Dunia nchini Qatar kwa kuongeza mauzo ya nyama katika jimbo la Ghuba kwa mwezi mzima wa michuano hiyo.
Taarifa kutoka Bodi ya Nyama nchini imesema asilimia 30 ya nyama kutoka Tanzania iliyouzwa nje mwezi Novemba ilikwenda Qatar ikiongeza mauzo ya tani 1,432 sawa na 125% kutoka tani 632 zilizouzwa nje mwezi Oktoba.
Qatar inaongoza kwa ununuzi wa nyama nchini Tanzania hasa ya mbuzi ikifuatwa na Oman, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Bahrain.
Nchi nyingine ni Kenya, Togo, Kuwait, China, Comoro na Canada.