TCRA yaanza vita dhidi ya warusha maudhui ya ushoga

HomeKitaifa

TCRA yaanza vita dhidi ya warusha maudhui ya ushoga

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema inaanza kufanya uchunguzi wa vituo vyote vya luninga na mitandao ya kijamii inayorusha maudhui ya katuni zinazohamasisha mapenzi ya jinsia moja kwamba hayaendani na maadili ya Kitanzania.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Habbi Guzne, Mjumbe wa kamati hiyo, Jacob Tesha alisema kamati imepewa mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 27(3)(a) cha Sheria ya Tcra.

“Siku za karibuni kumekuwa na taarifa inayosambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii yenye maudhui yanayohamasisha mapenzi ya jinsia moja kinyume na sheria, kanuni, maadili na miiko ya utangazaji nchini,

“Kamati inaviagiza vyombo vyote vya utangazaji nchini ikiwemo mitandao ya kijamii kuzingatia matakwa ya sheria, kanuni na masharti ya leseni ya utangazaji kwa kuhakikisha vituo haviendi kinyume na misingi ya utangazaji hasa kuepeka kutangaza maudhui yasiyofaa kwa jamii na hususani watoto,” alisema Tesha.

Aidha, alisema ni wajibu wa jamii nzima ikiwemo wazazi,viongozi wa dini na walimu ambao watoto hutumia muda mwingi wakiwa masomoni, kuhakikisha wanalinda watoto dhidi ya maudhui yasiyofaa.

error: Content is protected !!