Arsenal iliweka dau la pauni milioni 34 dirisha kubwa la usajili msimu huu kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania na Real Madrid, Marco Asensio (25) lakini ofa hiyo ilikataliwa (Cadena Ser, Mirror).
Mchezaji wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez anaweza kuchukua nafasi ya kocha wa sasa Ronald Koeman, kutokana na shinikizo la mashabiki wa klabu hiyo (Marca – Spanish).
Antonio Rudiger anaweza kupata mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki ikiwa ataondoka Chelsea, Bayern Munich na Juventus zipo tayari kumpa ofa hiyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 28 kwa sasa anapokea Pauni 130,000 kwa wiki kutoka Chelsea (Mirror).
Borussia Dortmund wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 25, kama mbadala wa Erling Haaland, 21 endapo ataondoka (90min).
Manchester City wanatazamiwa kuipiku Real Madrid kupata huduma ya mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe (22) msimu ujao (Transfer Window).
Atletico Madrid ipo mbioni kumsajili fowadi wa Arsenal, Bukayo Saka (20) (La Razon, Star).
Chelsea itaendelea na harakati zao kufuatilia upatikanaji wa mlinzi wa Sevilla, Mfaransa Jules Kounde, 22, na beki wa kati wa PSG wa Brazil Marquinhos, 27 (The Star)
Barcelona inaangalia uwezekano wa kumuuza mchezaji wao mbrazil Philippe Coutinho (29) katika dirisha dogo la usajili la Januari (Marca – Spanish).
Juventus wapo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina Paolo Dybala, 27, juu ya mkataba mpya na wamempa ofa mpya iliyoboreshwa (Kalciomercato – Italian).