Utaratibu mpya wa NHIF wasitishwa

HomeKitaifa

Utaratibu mpya wa NHIF wasitishwa

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesitisha mara moja utaratibu mpya wa matibabu uliotolewa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulioanza kutumika Tarehe 1 Agosti, 2022 kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini ambao unaweka zuio la idadi ya mahudhurio kwenye vituo vya kutoa Huda za Afya pamoja na utoaji wa kibali kwanza kabla huduma kwa mteja wa NHIF kwa vipimo vya MRI, CT SCAN, Colonoscopy, HBA 1C, OGD, USS na ECHO.

Waziri Ummy amesema pamoja na dhamira nzuri ya NHIF ya kutaka kudhibiti udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya vituo vya kutoa huduma za afya nchini na hivyo kuuweka mfuko katika hatari ya kufilisika, hivyo ameitaka NHIF kukaa pamoja na wadau wote ili kujadili na kuja na namna nzuri ya kuboresha utaratibu huo bila ya kumuathiri mteja pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.

Wizara ya Afya inapenda kuwahakikishia wanachama wa NHIF na wananchi kwa ujumla kuwa itafanyia kazi mapendekezo yote yatakayotolewa na kuja na njia nzuri ili kutimiza dhamira ya serikali ya utoaji wa huduma bora za afya kuanzia vituo vya afya ngazi ya msingi hadi Taifa.

error: Content is protected !!