Timu za soka kongwe zaidi Tanzania

HomeMichezo

Timu za soka kongwe zaidi Tanzania

Mchezo wa soka umekuwepo Tanzania miaka mingi kabla ya uhuru. Japo inaelezwa kwamba kulikuwa na timu nyingi hapo kabla, historia za timu nyingi zimeandikwa kuanzia miaka ya 1930. Kwa kutazama makabrsha ya historia tuliyopitia hapa Click Habari, zifuatazo ni timu kongwe zaidi Tanzania:

5. Mwadui FC
Ni timu iliyopo mkoani Shinyanga, ambayo iliazishwa katika migodi ya almasi. Ilitamba sana kwenye Ligi Kuu Tanzania bara miaka ya 1970 kabla ya kushuka daraja miaka ya 1980. Iliazishwa rasmi  mwaka 1955 hivyo sasa ina miaka 55.

4. Coastal Union
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mwaka 1988, wanatambulika kwa jina la ‘Wagosi wa Kaya,’ wakiwakilisha mkoa wa Tanga. Ni timu iliyozaliwa baada ya kundi la watu kujitenga kutoka kwenye timu ya African Sports yenye makao yake makuu barabara ya 12 jijini Tanga. Coastal yenye makao yake makuu katika barabara ya 11, ilianzishwa mwaka 1948 hivyo ina miaka 73 sasa.

3. Simba SC
Ilianza ikiwa na jina Queens FC, baadaye ikaitwa Sunderland kabla ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume kusema waachane na jina hilo la Kingereza. Ndipo ikaitwa Simba, ambapo iliazishwa rasmi mwaka 1936 na hivyo kwa sasa ‘Wekundu’ hao wa Msimbazi wana miaka 85.

2. African Sports.
Wanatambulika zaidi kama ‘Wanakimanumanu,’ na mwaka 1988 walitikisa zaidi walipobeba ubingwa wa Kombe la Muungano na kuiwakilisha nchi Klabu Bingwa Afrika. African Sports ya Tanga iliazishwa kabla ya Simba ya Dar es Salaam lakini zote zilianzishwa mwaka 1936. African Sports ina miaka 85.

1. Yanga SC.
Wengi wanafahamu kuwa ilianzishwa mwaka 1935, lakini historia ya kuanzishwa kwake inaanzia miaka ya 1910 ambapo vijana (wengi wakiwa wafanyakazi wa bandari) waliokuwa wwakifanya maazoezi kwenye viwanja vya Jangwani walipoanzisha timu na kujiita Jangwani Boys. Mtiririko wa matukio ulifuata, nikiwemo timu kubadilishwa majina na kuitwa Navigation, Italiana FC na New Youngs.Mgogoro wa mwaka 1935 ulipelekea wanachama kujiuzulu, waliobaki wakaanzisha Young Africans (Yanga), na walioondoka wakaanzisha Queens FC mwaka 1936, ambayo ndiyo Simba SC ya leo. ‘Timu ya Wananchi’ ina miaka 87.

error: Content is protected !!