Tinubu ashinda urais Nigeria

HomeKimataifa

Tinubu ashinda urais Nigeria

Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imemtangaza mgombea wa chama tawala APC, Bola Tinubu kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.
 
Tinubu amewashinda wagombea wengine 17 walioshiriki uchaguzi huo.
 
Tinubu amepata jumla ya kura 8,794,726, idadi kubwa zaidi ya wagombea wote, hivyo kukidhi matakwa ya kwanza ya kikatiba ya kutangazwa mshindi.
 
Pia amepata zaidi ya asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo 30, zaidi ya majimbo 24 yanayohitajika kikatiba.
 
Mwenyekiti wa INEC, Mahmood Yakubu ambaye ametangaza matokeo ya mwisho leo Jumatano mjini Abuja, amesema Atiku Abubakar wa PDP ameshika nafasi ya pili katika uchaguzi huo.
error: Content is protected !!