TRC yaomba nauli iongezeke kwa 15%

HomeKitaifa

TRC yaomba nauli iongezeke kwa 15%

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA-CCC), limesema limepokea maombi ya ongezeko la nauli za treni kwa asilimia 15 kwa kila daraja kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), kutokana na kupanda kwa bei za mafuta.

Hata hivyo LATRA-CCC imesema haioni kama kuna haja ya ongezeko hilo huku Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA) kikitaka shirika hilo lijikite kuboresha huduma zake.

Katibu Mtendaji wa LATRA-CCC, Leo Ngowi, alisema baada ya kupokea maombi hayo, walifanya utafiti mikoa mbalimbali.

Ngowi alisema wamefanya utafiti katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na Arusha na kubaini kuwa licha ya TRC kuhitaji ongezeko hilo la nauli, huduma zake hazikidhi mahitaji ya abiria kutokana na mabehewa mengi kupata ajali.

“Kutokana na upungufu huu, wananchi wamependekeza badala ya TRC kupeleka maombi ya kuongeza nauli, kwanza waboreshe huduma zao,” alisema Ngowi.

error: Content is protected !!