Treni ya mchongoko yawasili

HomeKitaifa

Treni ya mchongoko yawasili

Serikali imepokea seti ya kwanza ya treni ya umeme ya ‘Electric multiple unit’ (EMU) yenye vichwa vitano mchomoko na mabehewa matatu, Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa amesema.

Akizungumza wakati wa kukagua seti hizo katika Bandari ya Dar es Salaam, Mbarawa amesema serikali imeagiza seti 10 ya vichwa hivyo, ambavyo vitagharimu dola za Marekani milioni 190.

Mbarawa amesema kila seti moja ya kichwa itafunga mabehewa manane, yatakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 589.

“Leo tumepokea seti ya kwanza na kila mwezi tutaendelea kupokea seti hizi mpaka zitakapokamilika, ambazo zote kwa ujumla ni seti 10,” amesema Mbarawa.

Mbarawa amesema treni hiyo itakuwa na uwezo wa kutembea kasi ya Kilometa 160 kwa saa, ambapo amesema kabla ya kuanza kufanya kazi kwa seti hizo zitafanyiwa majaribio.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Amina Lumuli amesema ushushaji wa seti hizo ulianza Machi 1, mwaka huu katika bandari hiyo, hata hivyo kilichobaki ni kujiandaa kwa ajili ya majaribio na baadaye kutoa huduma.

“TRC tuko tayari kuanza kwa ajili ya kutoka huduma bora kwa wananchi, tunajiandaa tunaendelea kufanya maandalizi ya operesheni zetu,” amesema Lumuli.

Amesema hadi sasa wameshapokea mabehewa 65 na vichwa tisa yakiwemo seti ya kwanza ya EMU.

 

error: Content is protected !!