Rais Samia : Ripoti ya CAG ipatiwe majibu

HomeKitaifa

Rais Samia : Ripoti ya CAG ipatiwe majibu

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kuhakikisha wanapitia na kufanyia kazi ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kujibu hoja zilizotolewa.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapisha viongozi wateule wa ngazi mbalimbali za uongozi nchini

“Ripoti ya CAG ikafanyiwe kazi na hoja zijibiwe haraka ‘immediately’,” amesema  Rais Samia.

Hivi karibuni wakati akipokea Ripoti ya CAG, Rais Samia alielezea umuhimu wake kwamba zina mchango mkubwa sana kwenye maboresho mbalimbali yanayoleta maendeleo nchini.

error: Content is protected !!