Prof. Mohamed Janabi ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili (JKCI) amesema takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni nane hupoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na kuathiriwa na matumizi ya tumbaku huku akieleza kuwa kati ya wagonjwa 100 wanaougua moyo 25 kati yao chanzo ni tumbaku.
“Sigara zinawaathiri anayevuta na aliye karibu na anaye vuta, mke, mume au watu wanao kuzunguka na ubaya zaidi watu milioni nane hupoteza maisha kila mwaka na wakati Uviko-19 watu milioni tano ndiyo wamepoteza maisha duniani,” alisema Prof. Janabi.
> Ushahidi wa maboksi ya fedha kwenye kesi ya Sabaya
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa TTCF ameiomba serikali kupandisha bei za sigara ili kudhibiti matumizi ya bidhaa hzio kwa kuwasilisha bungeni muswada wa kudhibiti tumbaku unaokidhi matakwa ya Mkataba wa Kudhibiti Tumbaku wa Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO, FCTC).
“Bei za sigara zipo chini sana kulinganisha na mataifa mengine, naiomba serikali ipandishe bei kwa sababu wavutaji ni vijana na watu maskini hawatamudu gharama na matumizi yatapungua,” alisema Lutgard.