Uchumi kukua kwa 5.2% mwaka 2023

HomeKitaifa

Uchumi kukua kwa 5.2% mwaka 2023

Uchumi wa Tanzania unatarajia kukua kwa kasi ya asilimia 5.2 mwaka 2023 kutoka asilimia 4.7 mwaka jana ukichochewa zaidi na sababu mbalimbali zikiwemo ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za biashara na uwekezaji na kuimarika kwa utoshelevu wa chakula.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge leo jijini Dodoma kuwa matarajio hayo ya ukuaji yatatokana pia na uwezo wa kuhimili athari za kushuka kwa uchumi wa dunia, uwepo wa amani, usalama, umoja na utulivu ndani ya nchi yetu na nchi jirani na kuendelea kuimarika kwa viashiria vya ustawi wa jamii.

Dk. Nchemba amesema wanatarajia kuwa kasi ya mfumuko wa bei kuwa ndani ya asilimia 3 hadi 7 kwa kipindi cha muda wa kati huku nakisi ya bajeti ikitarajiwa kuwa chini ya asilimia 3 ya Pato la Taifa katika mwaka wa fedha wa 2023/24.

Mapato ya ndani yanatarajiwa kufikia asilimia 14.9 ya Pato la Taifa katika mwaka 2023/24 kutoka asilimia 14.4 mwaka 2022/23. Mapato ya kodi kufikia asilimia 12 ya Pato la Taifa kutoka matarajio ya asilimia 11.5 mwaka 2022/23,” amesema.

Hata hivyo, vita kati ya Urusi na Ukraine imeendelea kuathiri ukuaji wa uchumi katika nchi nyingi duniani hasa baada ya kuvuruga mnyororo wa thamani wa sekta ya uchukuzi.

Uchumi wa Tanzania umeanza kuimarika tena baada ya kuathiriwa vibaya na athari Uviko-19 mwaka 2020 na 2021.

Katika mwaka 2022, Dk Nchemba amesema pato ghafi la Taifa kwa bei za mwaka 2015 lilifikia Sh 141.9 trilioni kutoka Sh135.5 liliripotiwa mwaka 2021, sawa na ukuaji halisi uchumi wa asilimia 4.7.

Uchumi wa Tanzania umeanza kuimarika tena baada ya kuathiriwa vibaya na athari Uviko-19 mwaka 2020 na 2021.

Katika mwaka 2022, Dk Nchemba amesema pato ghafi la Taifa kwa bei za mwaka 2015 lilifikia Sh 141.9 trilioni kutoka Sh135.5 liliripotiwa mwaka 2021, sawa na ukuaji halisi uchumi wa asilimia 4.7.

Ukuaji huo, kwa mujibu wa Dk Nchemba ulitokana na mikakati ya Serikali kukabiliana na vita ya Ukraine, uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, barabara, reli na viwanja vya ndege.

Sekta zilizokuwa na kiwango kikubwa cha ukuaji mwaka 2022 ni pamoja na sanaa na burudani iliyokua kwa asilimia 19, madini (asilimia 10.9), fedha na bima (asilimia 9.2), malazi na huduma ya chakula, (asilimia 9) na umeme iliyokua kwa asilimia 7.6.

 

error: Content is protected !!