Ujinga sasa basi, DAR ES SALAAM sio ‘Bandari Salama’, hii ndio maana yake.

HomeElimu

Ujinga sasa basi, DAR ES SALAAM sio ‘Bandari Salama’, hii ndio maana yake.

Walio wengi wanatambua kuwa ‘Dar Es Salaam’ ni neno la lugha ya kiarabu likimaanisha ‘Bandari Salama’ huu ni upotofu uliodumu kwa muda mrefu sana, labda sio makosa yetu, ni makosa ya waliotufundisha.

Hata hivi leo ukimuuliza mtoto wa shule ya msingi juu ya maana ya neno Dar es Salaam atakwambia ‘Bandari Salama’. Swali hapa ni nani alianzisha hiki kitu, na ilikuwaje miaka yote hiyo hakuna mamlaka ambayo imejitokeza kuiweka sawa maana hii kutuokoa dhidi ya ujinga tuliolishwa na unaozidi kulishwa kwa watoto wetu na vizazi vijavyo.

Sasa basi, Kiarabu ni lugha na moja ya lugha maarufu sana duniani, ipo mitandaoni na njia na nyenzo rahisi sana za kuisoma lugha hii. Ukweli ni kwamba Dar es Salaam sio ‘Bandari Salama’ kama ijulikanavyo na walio wengi, hata ukaribu na maana ya bandari haina.

Neno ‘Dar’ kwa lugha ya kiarabu ni ‘Nyumba’ (Home), neno ‘Dar’ ukiacha ‘Salaam’ tunapata ‘Nyumba’. Halafu ‘Salaam’ ni ‘Amani’ kwa lugha hiyohiyo ya ‘kiarabu’. Hivyo basi unapata maana ya Dar es Salaam ni ‘Nyumba ya Amani’.

Ipo aya kwenye Qur an tukufu inasema (6:127) : لَهُمْ دَارُ ٱلسَّلَٰمِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Ukifuatilia hii aya kwa neno ‘Dar es Salaam’ limetajwa kama lilivyo, maana ya aya hiyo ni:

“For them will be the Home of Peace with their Lord. And He will be their protecting friend because of what they used to do”.

Mfano, kuna mji unaitwa ‘Dar’fur’ huko Sudan, pia ni muunganiko wa maneno mawili, ‘Dar na Fur’, ‘Dar’ nyumba na ‘Fur’ ni kabila kubwa sana katika mji huo, hivyo kutupa maana ya mji huo kama ‘Nyumba ya Fur’. Walio waislamu au kwenye kufahamu lugha ya kiarabu itakuwa tuko pamoja kwenye hili, kwenye sehemu nyingi hasa kwa mkoa wa Tanga ambapo naandika andiko hili, sehemu za kufundishia dini (Qur an) au Madrasa nyingi, zina majina yanayo anza na “ Darul”.. kama “Darul-Tahfidhul Quran” “Darul Uloomi” na kadhalika, ila hizi “Dar-ul” zote zikimaanisha ‘Nyumba’.

Sasa ilikuwaje Mzizima ikaitwa Dar es Salaam, hii ni hadithi inahusika moja kwa moja utawala wa ngome ya Ottoman katika harakati za kusambaza dini ya Kiislamu Afrika Mashariki, ugomvi na kanisa la Kilutheri na kadhalika. Baki nasi hapa clickhabari ambapo tutakuletea muendelezo wa historia hii.

error: Content is protected !!