Rais Samia aeleza ukuaji sekta ya fedha

HomeKitaifa

Rais Samia aeleza ukuaji sekta ya fedha

Katika mkutano wa 20 wa taasisi za fedha ulioandaliwa na Benki kuu ya Tanzania (BOT), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu ambaye alikua mgeni rasmi katika mkutano huo. Rais Samia ameainisha maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya fedha katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru.

Katika kutaja mafanikio hayo Rais Samia amesema Tanzania imefanikiwa kuwa miongoni mwa nchi kumi za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi lakini pia Tanzania kumekua na utulivu wa mfumuko wa bei na thamani ya pesa ukilinganisha na nchi zingine za Afrika.

Katika kuangalia viashiria vya maendeleo ya mtu mmoja mmoja Tanzania inaonekana inapata maendeleo ya mtu kwani kumekua na upungufu wa umaskini kutoka asilimia 28.6 mwaka 2015 hadi asilimia 26.2 mwaka 2020 na kwenye human Index kumekua na ongezeko kutoka 0.37 mwaka 1990 hadi 0.52 mwaka 2018.

Lakini pia Rais Samia alisema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru Tanzania imefanikiwa kuingia katika uchumi wa kati Julai 2020, Rais Samia amesema ni kutokana na kuwepo na sera nzuri na mipango bora kwaajili ya maendeleo lakini pia kuongeza mapato kupitia mifumo ya kidigitali.

Sambamba na hayo Rais ametaka Benki kuu ya Tanzania kuendelea kushirikiana na taasisi za mabenki, kutafuta mbinu bora ya namna gani watapunguza riba ili kuwezesha taasisi binafsi ziweze kukopa katika mabenki. “Tumemsikia mwenyekiti wa mabenki Tanzania kwamba na mabenki nayo tayari yameshaingia kwenye huo mfumo, na karibuni hivi tutasikia mkitangaza jinsi mnavyoshusha riba ili private sector iweze kukopa na wote tuendelee na maendeleo ya nchi yetu”

error: Content is protected !!