Umeme kitendawili, Makamba ashuhudia uhafifu wa maji Ruaha

HomeKitaifa

Umeme kitendawili, Makamba ashuhudia uhafifu wa maji Ruaha

Waziri wa Nishati Mhe January Makamba ameanza ziara katika mito inayoingiza maji katika mabwawa ya vituo vyote vya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji, ziara hiyo katika maeneo ya mito ililenga kutathimini hali iliopo pamoja na uzalishaji umeme ili kupanga mbinu za haraka za kukabili tatizo la upungufu wa umeme.

Katika Ziara hiyo Waziri Makamba aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la umeme Tanzania Maharage Chande, Bwana Maharage alisema kwamba shirika linachukua hatua za haraka kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia kwa kuharakisha matengenezo ya baadhi ya mitambo yake ya Ubungo I (MW 25), upanuzi wa Kinyerezi I (MW 185) na Ubungo III (MW 185).

Waziri Makamba ameshuhudia mtiririko hafifu katika mto Ruaha na kukauka kwa kwa mito midogo inayochangia maji katika mto Ruaha na katika bwawa dogo la Kidatu, Upungufu huo wa maji unachangiwa na ukame na uharibifu wa vyanzo vya maji hali iliyopelekea upungufu wa Megawati 307 kati ya Megawati 561 zinazopaswa kuzalishwa.

error: Content is protected !!