UN yaisifu Tanzania kwa kuwa na mifumo imara ya maridhiano

HomeKimataifa

UN yaisifu Tanzania kwa kuwa na mifumo imara ya maridhiano

Rais Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Amina Mohammed, ambaye ameisifu Tanzania kwa uimarishaji mifumo ya utatuzi wa changamoto kwa mazungumzo na maridhiano.

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao ambavyo Rais Samia na wasaidizi wake wamekuwa wakivifanya na viongozi mbalimbali wa jumuiya za kikanda na kimataifa, kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kimataifa.

Pia, Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameshakutana na Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres.

Katika kikao hicho, Amina aliisifu Tanzania kwa kuimarisha mifumo ya taasisi na utatuzi wa changamoto kwa njia ya mazungumzo na maridhiano.

Aidha, mazungumzo hayo pia, yamegusia mageuzi ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, ushiriki wa vijana katika maendeleo na umuhimu wa kuimarisha uratibu kati ya UN na AU.

error: Content is protected !!