Kwenye maisha kuna muda unajikuta kwenye changamoto ambazo hujui utatokaje, changamoto za kuonewa, kuendeshwa na kunyanyaswa zimekuwa nyingi kuanzia kwenye familia, kazini na hata kwenye uhusiano.
Zifuatazo ni dalili za kujua kama unapitia tatizo hilo;
Kulaumiwa kwa makosa ya watu wengine
Ikitokea kuna changamoto yoyote wewe ndo utatajwa kama msababishaji na utatakiwa kufanya chochote kuhakikisha unamaliza hiyo changamoto sambamba na hayo unapotokea ugomvi utahisi kuchanganyikiwa na hasira.
Mawazo yako kutosikilizwa
Mtu anaepelekwa hapewi nafasi ya kuongea kwani huogopa asije akaongea hisia zake hata kama kuna kitu kingine tofauti alikua anataka kuongea. Kuwa mtu wa kuitikia kwenye kila kitu
kwa sababu umetengenezewa mazingira ya kuogopa na kuwa upande wao kwenye kila kitu hta ikitokea kuna kitu unataka kukataaa utashindwa hivyo itabidi ukubaliane nao, kuna muda watakukejeli na kukwambia ni utani pia utakubali kwa sababu wamekutawala hauwezi kufanya maamuzi.
> Kamwe usimfanyie mwanaume mambo haya matatu
Watakutishia kusitisha vitu walivyokuwa wanakupa
Kama ni kazini utatishiwa kutokupewa au kupunguziwa mshahara, kwenye familia utatishiwa kufukuzwa au kunyiwa mahitaji muhimu na kwenye urafiki au mahusiano unaweza ukaachwa kupewa hela ili tu kukufanya ukubaliane na kila wanachosema.
Kujiona mwenye hatia na haustahili
Kwenye kila kosa unalofanya wao hutumia kama mtaji wa kukuumiza zaidi hivyo inakufanya hukose kujiamini na kukufanya hujihisi mkosaji kwenye kila unachofanya hali inayosababisha uchungu na majuto. Ni ngumu sana mtu kutoka kwenye mahusiano ya namna ila unatakiwa kujipa muda na kujaribu kutafuta mbinu sahihi za kujikomboa, jiwekee mipaka usiwe mtu wa kuwategemea kupata furaha na hakikisha unawaambia ukweli juu ya wanachofanya kuwa si sahihi itakusaidia kupata ahueni moyoni.