Upandikizaji Uboho sasa kufanyika Muhimbili

HomeKitaifa

Upandikizaji Uboho sasa kufanyika Muhimbili

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imeanza rasmi upasuaji na upandikizaji wa uboho( jina la kitaalam, Bone Marrow, ni ute unaopatikana ndani ya mifupa mirefu katika mwili wa binadamu huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuzalisha chembechembe za damu ambazo zina kazi mbalimbali mwilini) hatua inayoleta matumaini mapya kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na saratani. Hii inajulikana kama upandikizaji wa seli ya shina kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo ya upandikizaji wa Uboho nchini Tanzania, Mkuu wa  Kitengo cha Hematology na daktari bingwa wa magonjwa ya damu MNH, Dk Stella Rwezaula alisema hospitali hiyo hadi sasaimeshafanya upasuaji kwa wagonjwa watano na wengine watano wanaendelea kusubiri katika orodha.

“Ulikuwa ni mchakato mrefu uliohusisha wataalam mbalimbali wa afya kutoka idara mbalimbali kuhakikisha upandikizaji wa uboho unafanikiwa na unatunzwa vyema. Tulifanya kazi kwa pamoja na tunafurahi kwa hatua tuliyopiga kama taifa,” alisema Dk. Rwezaula.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema kuanza kutolewa kwa huduma hizo kutasaidia kila mgonjwa kuokoa karibu shilingi milioni 180 kama ataenda kutibiowa India, Kwani Mgonjwa hutumia shilingi milioni 250 kufata matibabu nje hususani India lakini MNH mgonjwa mmoja analipa takribani shilingi Milioni 70.

error: Content is protected !!