Vanessa Mdee adai kutolipwa na Standard Chartered

HomeKitaifa

Vanessa Mdee adai kutolipwa na Standard Chartered

Aliyewahi kuwa nyota wa muziki nchini Tanzania, Vanessa Mdee a.k.a Vee Money amewataka wasanii na watu maarufu nchini kuwa makini na kampuni zinazowachukua na kuwatumia kama mabalozi wa bidhaa na huduma zao kwani yeye mpaka sasa hajamaliziwa pesa na benki ya Standard Chartered tangu aanze kufanya nayo kazi mwaka 2019.

“Artists na watu maarufu Tanzania please don’t let these corporate companies take advantage of you. Mpaka leo lile benki halijamaliza kunilipa. Japo kiukweli ni benki bora but wameona wajikaushe. Yote kheri,” ameandika Vanessa Mdee.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Vanessa alitoa taarifa hiyo huku akionyesha kukubaliana na hali hiyo yakutomaliziwa kwa malipo yake kutoka kwa benki hiyo maarufu duniani.Hivi karibuni kumezuka malalamiko ya wasanii na watu maarufu kulalamika kuhusu makampuni kutowalipa au kumalizika kwa malipo mfano Riyama Ally na kampuni ya Unga wa kupikia ya Camel.

error: Content is protected !!