Usafiri wa mwendokasi Mbagala kurejea Novemba 20

HomeKitaifa

Usafiri wa mwendokasi Mbagala kurejea Novemba 20

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameziagiza kampuni ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka (UDART) pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali zilizo chini ya Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 20 mwezi huu, huduma za usafiri wa mwendokasi zirejee katika Barabara ya Mbagala kuelekea katikati ya jiji.

Chalamila ametoa maagizo hayo leo, Novemba 18, 2025, wakati alipotembelea vituo vya mabasi ya mwendokasi katika njia ya Mbagala pamoja na kukagua miundombinu iliyoharibika kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025, zilizotokea siku ya Uchaguzi Mkuu.

Amesema kuwa kwa sasa Serikali inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa miundombinu ya umma na mali za watu binafsi, sambamba na kuwatambua walioathirika kiafya au kupoteza mali aidha amesisitiza umuhimu wa Watanzania kuweka kando hasira na kuendelea kulijenga Taifa kwa pamoja.

Kuhusu njia ya mwendokasi inayotoka Gerezani kuelekea Kimara, amesema Serikali inaharakisha urejesho wa huduma ili usafiri urejee katika hali ya kawaida haraka iwezekanavyo.

error: Content is protected !!