Hii inawakuta watu wengi kwenye mapenzi, mtakuwa mashahidi kwamba kuna muda kama mapenzi yanapungua kwa mwenza wako. Ili kuepuka hali hii ni vyema kila mmoja akawa mbunifu zaidi ili kulifanya penzi lenu liwe moto moto kila wakati. Moja ya eneo la kuzingatia, ni kitandani, yaani wakati wa tendo la ndoa. Kwa mantiki hiyo basi, ni vyema kujua kwamba, kuna mambo hatupaswi kufanya wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Usiweke shinikizo kwenye kufika kileleni
Kila mmoja anatamani kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa, ni tamanio la kila mmoja. Lakini kufika kileleni isiwe shinikizo kwani inaweza kuharibu starehe na mahusiano yenu. Kufika na kutofika kileleni ni matokeo ya vitu vingi ikiwamo maandalizi yenu na hata hali zenu za kiafya kwa siku hiyo. Hivyo basi, mmoja wapo anapokuwa na matarajio makubwa ya kufika kileleni na kisha isiwe hivyo, inaweza kuharibu furaha katika mapenzi yenu, hii ni nje ya ngono ambapo ni sehemu ya ngono.
Usiangalie muda
Tendo la ndoa ni zaidi ya tendo linalohitaji nguvu tu, bali akili na utulivu wa hali ya juu. Ukianza kumuonesha mwenza kuna una haraka wa kumaliza hasa wakati au baada ya tendo anaweza kuishiwa hamu na tendo hilo. Unapoamua kujamiiana na mwenza wako, basi angalau kwa muda ule akili na mawazo yako yawe katika eneo lile, hii inalinda na kujenga zaidi mapenzi hata baada ya tendo la ndoa, kwani kuna mapenzi baada ya tendo.
Usikae mtindo mmoja kwa muda mrefu
Ili kuburudika wakati wa tendo wa ndoa, basi ni vyema kutumia mitindo/style mbalimbali. Mitindo itategemea na maumbile yenu, kuchoka na hata aina ya eneo mnalotumia kufanya kitendo hicho. Mwenza wako anaweza kushindwa kukueleza ukweli kuhusu tabia ya kutobadili mitindo, ila anaweza kubadilika kwa kupunguza mapenzi kwako na hatimaye kutimka kabisa. Lakini si kila mmoja anazingatia vitu hivyo kwenye mapenzi, ila ukweli ni kwamba vina umuhimu wake na vinaweza kuongeza chachu kwenye mahusiano.
> Dakika zinatosha kumfikisha mtu kileleni
Kate Moyle mtaalam wa ngono na uhusiano wa LELO anakubali, akisema: “Mara nyingi wanandoa, au mpenzi mmoja katika wanandoa wanaweza kuogopa kwa kuongeza kitu kwenye maisha yao ya ngono.”Lakini anaonya na kusema msichezeane tu zungumzeni Kwani ni vizuri kuchanganya utaratibu.
Usinywe mvinyo kupitiliza
Mara nyingi wanawake hupendelea kunywa mvinyo kwa ajili ya kulegeza mwili kabla hajaingia kwenye kufanya ngono ila unashauriwa kunywa kiasi kidogo ili uweze kupata hisia kikamilifu lakini pia mpenzi wako atahisi uwepo wako kwasababu utakuwa unashiriki ipasavyo.
Usifanye mapenzi ukiwa na njaa au umeshiba sana
Waswahili waliwaza mbali sana kusema “Shibe mwana malevya njaa mwana mageleza”.. Ndio, kimoja wapo hapo kikizidi ni hatari kwenye kufanya tendo la ndoa. Ngono ni shughuli pevu, hivyo unapaswa uwe umekula chakula cha wastani, usiwe umeshiba sana au mwenye njaa sana. Kushiba sana si vyema kwani mtu anaweza kuingiwa na uvivu kabla ya tendo, au kuwa na njaa sana kutamfanya mtu achoke haraka hivyo kushindwa kufikia lengo la tendo.