Utafiti: Wanaolala muda huu hatarini kupata maradhi ya Moyo

HomeElimu

Utafiti: Wanaolala muda huu hatarini kupata maradhi ya Moyo

Utafiti mpya kutoka Chuo Kikuu cha Exeter umetoa muda mzur wa kulala kupunguza hatari ya kupata magonjwa/maradhi ya moyo.

Utafiti huu umechapishwa Novemba 9 2021, ambapo unasema kuwa kulala muda wa saa 4 au saa 5 usiku ni vyema kuna kuna uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo, ni tofauti ni kulala mapema au kwa kuchelewa zaidi.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Dk. Davis Plans, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Exeter.

Dr. Plans anasema kuwa, katika mwili mwa mwadamu kuna kitu kinaitwa “Circadian rhythm”, ni mabadiliko ya kiasili kwenye miili yetu ambayo hubadilika kulingana na majira ya masaa 24.

Mabadiliko haya kuchagizwa na mwanga na kiza, yaani kuchomoza na kuzama kwa jua. Kwa mfano, unapolala kuanzia saa sita usiku, na ukaaka mchana siku ya pili, unaongeza hatari ya kupata
maradhi ya moyo, licha ya kwamba haijulikani sababu ni nini hasa. Hii huathiri mimea, wanyama, wadudu na viumbe wengine.

Kuna muda binadamu lazima awe amelala na kuna muda ni lazima awe macho, usiku majira ya saa sita ni muda ambao chembe hai (Cells) huzalishwa na kuzalishwa kwa uchache sana majira ya mchana. Sasa kuharibu utaratibu huu kila siku kwa kuwa na majira ya kutoeleweka ya kuamka na kulala, kunachochea maradhi ya moyo.

Plans anasema kuwa, majibu ya utafiti wao yanaonesha kuwa kulala mapema sana au kwa kuchelewa zaidi baada ya saa 4 na 5, kuna uwezekano mkubwa wa mtu kuugua ugonjwa wa moyo.

Utafiti huu umehusisha watu 88,026 kutoka Uingereza, na taarifa za watu hao zimekusanywa wakati wakulala na kuamka asubuhi kwa kutumia kifaa maalumu kinachovaliwa kiganjani, zoezi hilo lilifanywa kwa kila mmoja katika kipindi ya miaka mitano na miezi saba.

Kati ya watu wote, watu walioshiriki 3,172 ambao ni sawa na 3.6% walionekana kuwa na maradhi ya moyo

Utafiti huo umeonesha kuwa wale wanaolala kuanzia saa tano usiku na kuendelea wako hatarini kwa 12% kupata maradhi ya moyo, na wale wanaolala chini ya nne usiku wako katika hatari kwa 24%.

Kwa upande wa wanawake imeelezwa kuwa wako katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa urahisi kuliko wanaume.

Dr. Plans amesema kuwa, “ni lazima binadamu awe na muda maalumu wa kulala, na iwe baina ya saa nne usiku au saa tano. Kulala baada ya saa sita usiku kunaongeza hatari za kupata maradhi ya moyo.

Mwanzo nilikwambia kuhusu “circadian rhythm”, kuchelewa kulala kuna haribu utaratibu wa mwili ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kuchelewa kuamka asubuhi hivyo kupoteza majira
maalumu ya mwili wa mwanadamu.

Utafiti huu hautoi sababu ni kipi husababisha kuwe uhusiano kati ya muda wa kulala ma maradhi ya moyo, licha ya hivyo, majira ya kulala kwa sasa yamekuwa ni sababu kubwa sana
inayohusishwa na maradhi ya moyo.

error: Content is protected !!