Tofauti na wanaume, asilimia kubwa ya wanawake hutumia muda mrefu sana kutafakari kabla ya kufikia maamuzi ya kuwasaliti wapenzi wao, na zipo ishara ambazo huonekana pale ambapo mwanamke wako yupo mbioni kukusaliti
Kwanza, anatoweka bila sababu. Anaanza kubadilisha vitu ambavyo vilikuwa ni mazoea bila sababu ya msingi na hawezi kukuambia ukweli kuhusu alipokuwa, kwanini simu yake haipatikani ama hata kwanini hakutafuti wala hajajibu meseji kwa wakati. Kila anachosema ni visababu ambavyo havijitoshelezi.
Utaanza kuona yupo bize kila mara muda ule ule ama siku ile ile ya wiki.
Pili, una ukaribu na rafiki wa kiume ambaye urafiki wao unaingiliana na mipango yenu. Unapomwomba muonana ama mfanye jambo na mara kwa mara anakuwa na mipango na mingine na rafiki yake huyo. Hata baada ya kumwambia mara kwa mara namna urafiki huo unakufanya ujisikie anashindwa kubalance na kutafuta muda na wewe. Kuwa makini kuna namna analiwazika zaidi akiwa na rafiki huyo na inaweza kupelekea kuchepuka au tayari walishachepuka.
Tatu, kuna baadhi ya marafiki akiwa nao hapokei simu. Ukimpigia akiwa na Musa hapokei kabisa, anakata simu ama anapokea na kukupa jibu fupi “nitakupigia” na hapigi hadi atakapofika nyumbani akiwa mwenyewe ndio akupigie. Pengine Musa hubadilika ghafla akisikia anaongea na wewe kwenye simu ama hukasirika.
Nne, anaanza kutumia vitu vyake. Ana rafiki wa kiume ambaye wapo karibu sana na pengine wanajuana kabla yako. Ghafla wanapeana nguo kama vile masweta, anaanza kutumia gari lake, mara aazime laptop yake au yeye amuazimishe laptop yake.
Tano, hawezi kuachana na rafiki ambaye amekua mwiba kwenye mahusiano yenu. Utajaribu kuongea nayelakini hayupo tayari kutokuwasiliana na huyo mtu. inawezekana ni ex wake ama rafiki wa kawaida ambaye hawajawekeana mipaka n hayupo tayari kuiweka. Kwenye mahusiano ya kufika mbali na kutengeneza familia, ni lazima baadhi ya watu wabaki chini ili kusudi nyie muweze kupanda na kufikia malengo yenu. nao wapande kwa namna yao.
Sita, anakuwa muongo kwa kila kitu. Kabla ya kukujibu huwaza jibu la kukupa. Na akirudia sana hiyo stori anaweza kuanza kusahau baadhi ya vitu alivyosema mwanzo. ama hataki kuongelea baadhi ya vitu kwa kusema havina maana kuzungumzia.
Mpe uhuru na usimnyime kuwa na marafiki bali pale tu ambapo rafiki zake wanaonekana kweli kumpotosha ama wanaweza kuharibu mahusiano yenu na sio tu kwasababu una wivu uliopitiliza.