Hali ilivyo kwa sasa ni kwamba Tanzania ni mnufaika mkubwa kiuchumi kutokana na mgogoro wa kibiashara unaoendelea kati ya Uganda dhidi ya Kenya na Rwanda.
Wiki hii, serikali ya Yoweri Museveni wa Uganda imetangaza vikwazo vya bidhaa za kilimo kutoka Kenya, hatua ambayo imechochea zaidi mgogoro wa kibiashara kwa
mataifa hayo mawili. Mgogoro wa kibiashara kati ya Uganda na Kenya umedumu kwa takribani miaka miwili sasa, mgogoro ambao ulipangwa kupata muafaka wake
mwezi uliopita lakini ahadi ya muafaka hiyo haikujiri.
Waziri wa anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Bi. Rebecca Kadaga aliamshirisha kuorodheshwa kwa bidhaa za kutoka Kenya
na kisha kuzipiga marufuku kwenye soko la Uganda huku akitoa onyo kwamba, “Ndani ya muda mfupi tu, Kenya wataelewa tunapitia wakati gani, tumewavumilia
muda mrefu sana Kenya, lakini uvumilivu wetu umefika mwisho”..
Huku ikiwa kwa sasa mgogoro kati ya Uganda na Rwanda umepoa kidogo, mgogoro ambao ulipelekea kufungwa kwa mpaka wa Katuna/Gatuna Februari 2019.
Wakati Uganda, Rwanda na Kenya wanavutana, kwa kipindi Tanzania imekua ikitumia mgogoro huu kwa maslahi yake kiuchumi tangu wakati Hayati Rais Magufuli.
Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri sana na Uganda katika siku za hivi karibuni, kuifanya Uganda kama sehemu muhimu zaidi kwa uwekezaji.
Disemba 9 wakati Tanzania ikiidhinisha miaka 60 ya Uhuru wake, mgeni rasmi alikuwa Rais wa Kenya Uhuru wa Kenyatta, Kenya alizuru Tanzania kama mgeni rasmi,
lakini pia alisalia siku mbili zaidi kwa ajili ya kutia saini makubaliano ya mkataba wa bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa.
Wiki tatu nyuma kabla ya maandimisho ya Uhuru, Rais Samia alifanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kufungua fursa za kiuchumi baina ya mataifa
mawili, Tanzania na Uganda hasa wakati huu ambapo janga la Korona limepungua kasi. Unaweza kuona namna Rais Samia alivyokuwa kimkakati katika kunufaika na
mgogoro kati ya Kenya na Uganda.
Mataifa yote ya Afrika ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaitazama Tanzania kwa karibu zaidi kama mshirika wa kibiashara kutokana na serikali ya Rais Samia kuondoa
vikwazo vya kibiashara ambavyo awali vilileta ugumu kuuza na kununua bidhaa kutoka Tanzania. Rais Samia hadi hivi sasa amefanya ziara katika nchini tano za
Jumuiya ya Afrika Mashariki isipokuwa Sudani Kusini.
Katika makutano yake na Uhuru Kenyatta Rais Samia alitangaza kuondoka vikwazo vya kibiashara kwa Kenya, vikwazo ambavyo viliwekwa na mtangulizi wake
Hayati Magufuli. Hatua hii imeirahisishia Kenya kufanya biashara, na ni wakati sahihi wa kuikacha Uganda na kuelekeza nguvu zake zote kwa Tanzania, hivyo
Tanzania inatarajia kuuza bidhaa nyingi zaidi za kilimo kuenda Kenya.
Machi mwaka huu Kenya iliweka vikwazo mahindi kutoka Uganda, hatua ambayo iliwakarahisha sana Uganda na Bunge lao kuazimia kulipiza kisasi dhidi ya Kenya,
hatua ambayo Museveni aliipinga na kusema kwamba kufanya hivyo ni kuharibu utaratibu wa soko la pamoja na Afrika Mashariki.
Hatua ya Uganda kulipiza kisasi kwa kuzuia bidhaa za Kenya, ni baada ya kuona hakuna dalili za muafaka na Serikali ya Uhuru kwenye kuachia mahindi ya Uganda
kuuzwa nchini Kenya.
Kenya ilikacha mazungumzo na Uganda yaliyolenga kujadili juu ya vikwazo vya bidhaa (Maziwa, Sukari) kutoka Uganda, ambapo Idara ya Mifugo kutoka aliitupia lawama
serikali ya Kenya kwa kuwa na maandalizi mabovu juu ya mkutano huo. Kutokufanyika kwa mkutano huo kunaendeleza mvutano uliodumu miaka miwili sasa
kati ya Kenya na Uganda juu ya bidhaa za Sukari na Maziwa.
Shutuma za Serikali ya Kenya dhidi ya Uganda kuhusu bidhaa za Maziwa na Sukari zinadai kwamba, Maziwa na Sukari kutoka Uganda sio bidhaa za Uganda, bali Uganda
hununua bidhaa hizo kutoka nje na kuiuzia Kenya kinyemela, shutuma ambazo Uganda imezikataa vikali.
Kenya imewekewa vikwazo na Uganda kwenye bidhaa kama Mafuta ya mchikichi ambapo mwaka jana pekee mafuta hayo yaliingizia Kenya dola milioni 64, ulezi dola milioni 12.4,na Mbogamboga dola milioni 2.77. Biashara kati ya Kenya na Uganda inaendelea kuzoroto zaidi tangu Aprili 2021, ambapo Kenya imeuza bidhaa zenye thamani ya dola za imarekani milioni 83.25, ikashuka hadi dola milioni 71 Mei, hadi kufikia Juni mwaka huu ikafika dola milioni 66.85.
Hatua hii imeifanya Tanzania kuipita Kenya kama nchi inayoongoza kufanya biashara na Uganda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mvutano wa Uganda na Kenya pamoja na Rwanda umeifanya Tanzania inufaika sana kibiashara. Kwa mfano, katika robo ya tatu ya 2021 biashara ya bidhaa za Tanzania kwenda Rwanda imeongezaka maradufu kwa asilimia 66.37, ikiwa ni tofauti na mwaka jana katika robo ya tatu ya 2020 ambapo biashara ilikuwa 61.18% kwa mujibu wa taasisi ya takwimu ya Rwanda (RIS)
Kenya ikiwa ndio nchi ya pili kufanya biashara na Rwanda baada ya Tanzania, biashara ya Kenya na Rwanda imepungua hadi 33.44% ambapo ni sawa na dola za kimarekani milioni 76.69 katika robo ya tatu ya mwaka huu, tofauti na mwaka jana ilikuwa 38.82.
Kenya inaweza kudhurika zaidi kibiashara kutokana na uchaguzi mkuu unaokuja nchini humo 2022, wafanyabiashara wengi wanaweza kuacha
kutumia bandari ya Mombasa kwa muda kutoka na historia ya vurugu cha uchaguzi zilizowahi kutokea mwaka 2007/08. Hapa Tanzania
ijiandae kupata faida kubwa sana kwenye biashara, mizigo ya Rwanda na Uganda itaingia kupitia bandari ya Dar es Salaam au Tanga.
Mgogoro wa Uganda na Kenya utashuhudia upotevu wa mapato ya dola za kimarekani 121. Uganda kwa sasa imeanza kukacha kutumia bandari ya Uganda kuingiza bidhaa zake imeelekeza nguvu zake bandari ya Dar, Rwanda nayo halikadhalika ilikuwa inatumia bandari ya mombasa kupita Uganda, inaanza kuancha na kutumia zaidi kutumia bandari za Tanzania kama Dar na Tanga, Rwanda Petroli yake kwa wingi kupitia Tanzania.