Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti amewataka waandishi wa habari kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa kuwaambia wao pia wapo katika makundi hatarishi kutokana na kukutana na watu wengi wanapokwenda kutekeleza majukumu yao.
“Nawashauri nanyi mchanje, maana mmo katika makundi hatari, mnapofanya kazi zenu mnakutana na wananchi wengi na viongozi pia, kwa maana hiyo salama yenu ni kuhakikisha mmechanja na kufuata taratibu zote za kujikinga, kama zinazoelekezwa na wataalamu,” alisema Mkirikiti.
> Utafiti: Namna Vitamin A inavyoweza kutibu tatizo la UVIKO-19
Aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari kuwaeleza mafanikio ya Serikali katika kipindi cha miezi sita tangu ilipoingia madarakani.
Pia amewataka waandishi kutumia vyombo vyao hasa redio, kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kupata chanjo hiyo, kwani zinatolewa bure.