Wabunge wa Pakistan wamepitisha sheria ambazo zitaruhusu kuharakishwa kwa kesi pamoja na adhabu kali dhidi ya wabakaji ikiwemo kuwawekea kemikali kwenye sehemu zao za siri. Watuhumiwa wataokutwa na hatia ya ubakaji watahukumiwa kifo au kifungo cha maisha na watakapopatikana na hatia ya kurudia watahasiwa kwa kutumia kemikali.
Wabunge hao wameridhia sheria hizo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kutokana na ongezeko kubwa la ubakaji wa wanawake nchini humo, Pia serikali inategemea kuanzisha mahakama maalum kote nchini ili kuharakisha kesi dhidi ya washukiwa wa ubakaji ikiwezekana ndani ya miezi minne kesi iwe imeshaamuriwa.
Pia bunge hilo lilipitisha sheria ya kuwepo kwa orodha ya kitaifa ya washukiwa wote wa dhuluma za kingono kwa msaada wa idara ya kitaifa ya kukusanya data, lakini pia taarifa kuhusu waathirirka zitakuwa siri wakati kukiwa na vyumba maalum vya kuwapatia ushauri pamoja na kuwapa huduma za kiafya muda mfupi baada ya kubakwa.