Wabunge waliopoteza imani kwa wananchi hali tete

HomeSiasa

Wabunge waliopoteza imani kwa wananchi hali tete

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza mabadiliko ya mfumo wa upatikanaji wa wagombea ubunge na udiwani kwa lengo la kuongeza ushirikishwaji wa wananchi na kuhakikisha wagombea wanaokubalika wanapitishwa.

Akizungumza mjini Tabora, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, alisema wabunge waliopoteza imani ya wananchi na kutowarudia hawatategemea msaada wa chama kwenye uchaguzi ujao. Alisisitiza kuwa chama hakitapitisha wagombea kwa mazoea bali kwa ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni.

Wasira alisema kuanzia Juni 28 hadi Julai 5, chama kitakuwa tayari kimebaini majina ya wagombea, huku akionya dhidi ya mbinu chafu na matumizi ya nguvu kwenye mchakato huo.

Aidha, aliwahimiza Watanzania kulinda amani na kutumia taasisi halali kama Mahakama kutafuta haki badala ya vurugu, akisisitiza kuwa “ndani ya amani kuna haki.”

error: Content is protected !!