Wadudu chini ya ngozi ya uso kama vile Demodex folliculorum hutumia maisha yao yote kuishi ndani kabisa ya uso wa mwanadamu.
Usiku, viumbe hao huondoka chini ya vinyweleo ili kutafuta ngozi mpya kwa kukutana na mpenzi au mwenzi.
Na ni shughuli hiyo ya wakati wa usiku ambayo inaweza kukufanya ugeuze mwili kutoka upande mmoja hadi mwingine.
“Usiku, tukiwa katika usingizi mzito, wanatembelea katika matundu ya vinyweleo ili kukutana kimwili na kupata watoto,” anasema Dk Perotti mmoja wa washiriki wa utafiti
Lakini utafiti mpya umegundua wadudu hao wanaweza kukabiliwa na tatizo kwani DNA yao inaharibika, kumaanisha kuwa wanakaribia kutoweka.