Waliopandikizwa  mimba wajifungua

HomeElimu

Waliopandikizwa mimba wajifungua

Wanawake watano kati ya tisa waliopandikizwa mimba kwa njia ya ‘IVF’ na ‘artificial insemination’  jijini Arusha wajifungua salama.

IVF ni njia ya uzazi ambapo yai la mama lililokomaa na manii huunganishwa maabara kutengeneza kiinitete kisha kurejenshwa na kushikizwa kwenye ukuta wa tumbo la uzazi ili mimba iendelee kukua. Huku insemination ni njia ya uzazi ambapo manii hutolewa kwa mwanaume, kusafishwa na kisha kuwekwa kwa moja kwa moja mfuko wa uzazi ili kumrahisishia kushika mimba.

Madaktari bingwa wazawa kutoka Avita Care, Arusha na Hospitali ya Taifa Muhimbili walishirikiana kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya uzazi kupata watoto kwa njia hizo mbili na watano kati yao kufanikiwa kujifungua watoto salama salmin.

error: Content is protected !!