Wamasai wamshukuru Rais Samia

HomeKitaifa

Wamasai wamshukuru Rais Samia

Wakazi wanaoishi katika Hifadhi ya Ngorongoro ambao wameamu kuhama kwa hiari eneo hilo na kwenda kuishi Msomera Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali  kwa kuweka mazingira na utaratibu mzuri wa kuwahamisha wao pamoja na mali zao kufika katika makazi mapya .

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa sababu ameonesha kutujali sana kwani Serikaliimetylipa fidia  lakini mama kwa huruma yake akatuongezea hivyo tumefarijika na tunaondoka tukiwa na amani kubwa moyoni na tunamwombea kwa Mungu Rais wetu na Serikali yake waendelee kufanya kazi na kutuletea maendeleo sisi wananchi,” ameeleza Samuel Huho (60) kutoka kijiji cha Kimba kilichopo eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa upande wake, Richard Olemoko wa Kijiji cha Mokilal anaeleza kuwa eneo la Msomera ni bora zaidi kuliko hifadhi kwa sababu anakwenda kuwa na makazi ya kudumu.

“Maisha ya hapa hayana uhakika na ukitaka kujenga mpaka kibali tena kwa masharti , sasa hayo maisha gani? Ninatoka eneo duni kwenda eneo bora zaidi. Kule nina nyumba nzuri niliyojengewa na serikali, shamba la kulima na kuna huduma zote za kijamii, nawashukuru viongozi wa serikali kuanzia Mheshimiwa Rais Samia, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na watendaji wote kwa kututhamini sisi tulioamua kuondoka kwa hiari,” anaeleza Olemokoloa ambaye ana mke na watoto wawili.

Jumla ya familia 27 kati ya 103 zilizoamua kuondoka kwa hiari eneo la Hifadhi ya Ngorongoro zinasafirishwa na Serikali katika awamu ya kwanza kuelekea Msomera, Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuanza makazi mapya ili kupisha uhifahdi katika eneo la Ngorongoro.

error: Content is protected !!