Kampuni ya Facebook, inayomiliki mtandao wa WhatasApp, imetangaza kuwa inaboresha mfumo wa programu tumishi wa WhatsApp hivyo kuwataka watumiaji wa baadhi ya simu za iPhone kufanya maboresho (updates) ya WhatsApp zao ili kuendana na mabadiliko hayo.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza, Apple imesema mchakato wa WhatsApp kuacha kutumika kwenye baadhi ya iPhone utaanza Novemba 1 2021, hivyo kila mmoja aboreshe WhatsApp yake mapema kuepuka kadhia.
Apple imetangaza kuwa iPhones zote zilizotoka nyuma ya mwaka 2016 zitakumbwa na kadhia hiyo, na baadhi ya mbele ya 2016, hivyo watu wanapaswa kuboresha WhatsApp zao angalau kwenye mfumo wa iOS 10.
Zifuatozo ni iPhone ambazo zinapaswa kuboreshwa ili kuendelea kutumia WhatsApp.
- iPhone 5
- iPhone 5C
- iPhone 5S
- iPhone 6
- iPhone 6 Plus
- iPhone SE (1st-gen)
- iPhone 6S
- iPhone 6S Plus
- iPhone 7
- iPhone 7 Plus
- iPhone 8
- iPhone 8 Plus
- iPhone X
- iPhone XR
- iPhone XS
- iPhone XS Max
- iPhone 11
- iPhone 11 Pro
- iPhone 11 Pro Max
- iPhone SE (2nd-gen)